TANZANIA: Jay Mo naye aongelea kuhusu suala la kufanya video nje ya nchi.

 

Baada ya hivi karibuni msanii wa muziki ya miondoko ya hiphop wa nchini Kenya Prezzo kuwaambia wasanii wa Tanzania wanaendea kufanya video ya nchini hususani nchini Afrika Kusini na kuwaasa kubaki nchini mwao ili kukuza soko la ndani la muziki.

Pia msanii mahiri wa miondoko ya hiphop wa nchini Tanzania Jay Mo amesikika katika kipindi cha XXL kinachorushwa na kituo cha habari cha Clouds Fm, Jay Mo alisema kwamba wasanii wengi wanaenda kufanya video nje  kwa mkumbo kwa kuona Fulani amefanya, pasipo kua na malengo yakinifu.

Aliendelea na kusema kuwa ni vyema wasanii wajue wanapoenda kufanya kazi nje wajue wanalenga soko la wapi, na sio kukurupuka. Hivyo msanii anaweza akafanya video ndani ya nchi na kuteka soko la ndani halikadhalika na la nje pia.

 

Leave your comment