TANZANIA : Diamond kuingiza ngoma mbili kwenye BBC chat ya Radio One Extra!

Msanii Diamond Platnumz amefanikiwa kuingiza nyimbo mbili kwenye Top 5 za Afro Boss Airline DNA  za kipindi cha Destination Africa kinachotangazwa na DJ Edu kupitia BBC Radio One Extra.

Ambapo nafasi ya kwanza ni wimbo aliofanya na rapa wa Afrika Kusini, AKA ‘Make Me Sing’ na Zigo Remix aliyoshirikishwa na AY imekata nafasi ya tatu.

Zigo Remix kabla ya kushika nafasi ya tatu ilishika nafasi ya kwanza , na huku jumatatu ya leo Harmonize ameachia wimbo mpya akiwa na Diamond Platnumz unaenda kwa jina la ‘Bado’.   

Leave your comment