Ukimya wangu ulinipa uwoga kurudi – Dogo Janja!

 

Rapa Dogo Janja kutoka Tip Top Connection amesema wimbo wake mpya wa ‘My Life’ ni muziki alioufanya kwa kuwa alikuwa anatafuta njia ya kurudi kwenye muziki baada ya ukimya wa muda mrefu.

Akizungumza katika kipindi cha Planet Bongo cha East Africa Radio ijumaa iliyopita, Dogo Janja alisema likuwa na wasiwasi kabla ya kuutoa wimbo huo.

“Kitu ambacho kilinifanya nichange style, nilikuwa nafukiria jinsi ya kurudi, pia nilikuwa muoga nikawa narekodi napeleka, narekodi napeleka, kuna jamaa anaitwa Cal kutoka Norway ni producer alikuja Bongo sasa walikuwa wamenitumia beat, nikaenda studio nikajikuta nimepata melody, michano, nikawatumia michano management yangu wakaona hii tuiboreshe , ndio ngoma ikatoka”, alisema Dogo Janja.

Leave your comment