Inasemekana maapenzi katika umri mdogo na ulevi husababishwa na muziki wa rap!
29 February 2016

Utafiti unaonyesha muziki wa rap ni chanzo kikubwa cha ulevi na mahusiano ya mapenzi katika umri mdogo. Kwa miaka mingi wanamuziki, wazazi na vyombo vya habari wametumia miongo mingi kujadili na kutafuta ufumbuzi wa jinsi filamu chafu zinavyoweza kuwa na athari kwa watoto.
Watafiti kutoka Houston, Marekani wamedai kuwa uhusiano wa moja kwa moja kati ya muziki wa rap na watoto wenye miaka 10 kujiingiza kwa mahusiano ya kimapenzi chini ya umri na unywaji wa pombe.
Utafiti huo ulihusisha wanafunzi 450, kwa muda wa miaka 2, na kubaini kuwa wale waliosikiliza muziki wa rap wakiwa gredi ya saba walikuwa na uwezekano wa kufanya mapenzi wakiwa gredi ya tisa.
Pia utafiti huo ulionesha kuwa muzkiki wa rap una uwezekano wa kuwa na picha zinazochochea mapenzi kuliko aina nyingine yoyote ya muziki.
Source: Daily Mail




Leave your comment