TANZANIA: Nay wa Mitego adai utajiri wake unathamni ya bilioni 1.

Msanii wa muziki wa hip hop nchini Tanzania Nay wa Mitego amedai na kusema hela pamoja na mali anazozimiliki zinathamani ya shilingi Billioni 1.

Akizungumza katika kipindi cha The Weekend Chatshow cha Clouds Tv , Nay alisema biashara pamoja na muziki ni vitu vinavyomuingiziza pesa  nyingi. “ Mimi na mali zangu na kila kitu zinifika kwenye billioni hivi. Ukichanganya hela zilizokuwa benki pamoja na biashara ninazofanya thamani yake zinafikia bilioni moja na kitu. Sitaki kudanganya watu sijue kwenye bilioni mbili huko.”

Rapa huyo mwaka 2014 alihamia kwenye nyumba yake iliyoko maeneo ya Mbezi jijini Dar es Salaam yenye thamani ya milioni 200.

Leave your comment