TANZANIA:Diamond adaiwa kukopi idea ya video

Msanii kabambe anayetambulika ndani na nje ya bara la Afrika Naseeb Abdallah "Diamond Platnumz" adaiwa kuiga idea ya wimbo wa 'Make me sing' kutoka kwenye nyimbo ya 'Got money' ya Lil Wayne.

 

 

Kutokana taarifa hizo Diamond ambaye ni baba wa mtoto Latifa amejibu na kusema kuwa, "watu wanashindwa kuelewa kila kitu ambacho kinafanyika katika muziki sasa kwenye video, kwenye kuimba, mashairi na vyote vilishafanyika, vimeshaimbwa ni kama marudio lakini kila mtu anarudia kwa namna yake anayoijua yeye." Nyimbo hiyo ambayo imekua ni gumzo barani Afrika na kutazamwa mara milioni 1 mtandaoni kupitia YouTube. 'Make me sing' ilitayarishwa na Tudd Thomas na kutengezwa na Nicky.

Leave your comment