TANZANIA: ‘Hewalla’ video imegharimu millioni 50 – Mzee Yusuph
25 February 2016

Mfalme wa muziki wa taarabu nchini, Mzee Yusuph amedai video yake ya wimbo wa ‘Hewalla’ aliyomshirikisha Vanessa Mdee imegharimu kiasi cha shilingi milioni 50.
Mzee Yusuph ameyasema hayo wakati akizungumza katika kipindi cha Uhondo cha E FM hivi karibuni, kuwa licha ya kupata kitu kizuri kutokana na gharama hiyo pia amejifunza vitu vingi.
“Kwa ufupi kuna vitu nimejifunza na nimeona sasa hivi nitafanya na director wa hapa nyumbani sio tena Afrika Kusini kwa nyimbo zangu zinazokuja, tena kwa kiwango kile kile ninachokipata Afrika Kusini. Kwasababu nimefikiria ukimlipa director wa hapa pesa za kutosha naweza pata ninachokihitaji. Kwasababu mil 25 imekuwa mara mbili, kwahiyo mil 50 imekwenda kwenye video moja, kwa kumtaka Vanessa tumsubirie tumelipia mara mbili, kwahiyo nikasema hawa director wetu sidhani kama itafika, tukimpa milioni 15 hawezi fanya kitu kweli? Tukalipia location na kila kitu”, alisema Mzee Yusuph.
Pia aliongeza, Hanscana nilimwambia nataka hiki na hiki akaniambia sawa na yule Msafiri wa Kwetu Studio nimemwambia nataka hiki na hiki. Kwasababu video ya wimbo Mahaba Niue watafanya Kwetu Studio halafu kaning’ang’ania atafanya Hanscana ili nilinganishe tuone nani ni nani kati yao, lakini nina imani watafanya vizuri kwasababu nimewatimizia yote”.




Leave your comment