Tanzania: "Heri msukuma mkokoteni kuliko msanii" - Ray C

 

 

 

Msanii wa muziki ya Zouk Rehema Chalamila maarufu kama Ray C amesema kuwa hawezi kutoka kimapenzi na msanii tena kwani hataki kuumizwa tena kama alivyofanyiwa na mpenzi wake wa zamani Lord Eyes.

Katika mahojiano yake na Enewz cha East Africa Television, mwanadada huyo alisema tangu alipokuwa kwenye mahusiano na msanii huyo Lord Eyes aliumizwa sana na hata kumpelekea kujiingiza katika madawa ya kulevya.

Ray C akiwa na mpenzi wake wa zamani Lord Eyes

 

"Kwa sasa bado sina boyfriend, kwakweli nafasi hiyo bado maana Lord Eyes ameniumiza sana. Nilimpenda sana na ndo maana nilikuwa nikfanya alichokua akifanya. Sikutegemea kama ingekua vile, hata kwenye drugs unakutana na rafiki yako anafanya hili na wewe unataka kufanya ili aone upo pamoja nae. Ila kwa sasa mimi na wasaniii hapana, ni bora hata nitoke na msukuma mkokoteni ili mradi anipende maana mimi ninamapenzi ya kweli, na ndio maana hata nyimbo zangu nyingi ni za mapenzi" - Alisema Ray C

Leave your comment