TANZANIA: “Siyataki mapenzi ya Instagram”- Dayna Nyange
25 February 2016

Msanii wa kike anayefanya vizuri katika industry hii ya muziki nchini Tanzania, Dayna Nyange anaetamba na nyimbo kama nivute kwako, angejua na nyinginezo amesema hataki mapenzi ya Instagram.
Katika mahojiano yaliyorushwa kupitia kipindi cha The One Show cha Tv 1 amesema kuwa kwa sasa hana mpenzi na hapendi kuweka mapenzi yake hadharani hasa kwenye mtandao wa Instagram.
Amisikika akisema kuwa hata ikatokea amekua kwenye mahusiano na wakaachan na kufanya maamuzi ya kuwa na mpenzi mwingine, jamii haitamchukulia vizuri bali ataishia kumuona kama muhuni ambavyo ni tofauti na atakavyochukuliwa mtoto wa kiume.
Hivyo msanii huyo amewasihi wasanii wenzake kuwa wasiri katika mahusiano yako, na pia amewaomba mashabiki wake wajiandae kwani amejipanga na ana nyimbo zenye ladha tofauti.




Leave your comment