TANZANIA: Prezzo awapa makavu wasanii wa bongo
25 February 2016

Msanii kutoka Afrika mashariki anayeitambulisha nchi ya Kenya kwa nyimbo zake za hip hop, Prezzo amesikika akiwapa makavu wasanii wa kitanzania wanaokimbilia kufanya video nchi za nje.
Amesikika akisema hayo kupitia kipindi cha Clouds E cha Clouds Tv kuwa wasanii wa bongo wamekuwa wakifwata mkumbo, wakiona mwenzao mmoja ameenda kufanya video nchi za nje na wao wanaiga wakiamini watafanikiwa.
Prezzo amewataka wasanii wa bongo kufanya kazi na waongozaji wa ndani, kwani kuna sehemu nzuri , na vitendea kazi ambavyo vitafanya kazi kwa ubora na kuwavutia wasanii wengine wa nje kuja na kuwekeza kwenye soko la ndani. Prezzo kwa hivi sasa yupo nchini kikazi akiambatana na menejimenti yake, ambapo ameshaanza zoezi la kutengeneza video yake itakayo kuja hivi karibuni chini ya muongozaji anae kuja kwa kasi Hascana kutoka Wanene Studio.




Leave your comment