TANZANIA: “Siwezi kutaka kiki kwa Linex”-Baraka Da Prince
24 February 2016

Msanii wa muziki wa bongo fleva, Baraka Da Prince amesema kuwa hawezi kutaka kiki kupitia Linex.
Hii yote imetokana na picha zilizosambaa mitandaoni kupitia Whatsapp zikionyesha Baraka da prince akiwa na mwanamke wa Linex. Kupitia kwa YOU HEARD ya Soudy Brown ya Clouds Fm Linex alisema,”Sijapaniki kwasababu dogo amefanya kitu cha kipuuzi, siyo sawa kabisa…. na yeye ni kama mdogo wangu”.
Baraka Da Prince naye hakukaa kimya, akajibu kupitia countdown ya Amplifaya ya Clouds Fm akisema,” Sijwahi kutembea na mtu anayetembea na Linex. Kwanza hawezi akatembea na mtu ninaye tembea nae mimi, yeye labda ndio anataka hito kiki ila mimi siwezi kutaka kiki kwa Linex… Linex kakosea”




Leave your comment