TANZANIA: Kufanya video nje ya nchi kunafanya wasanii kujifunza vitu vipya – Belle 9
24 February 2016

Msanii Belle 9 adai wasanii wanaenda kushoot video na waongozaji wa nje ili kujifunza na kutanua wigo wa muziki wao.
Belle 9 amesema kuwa wasanii kwenda kushoot video nje kunawafanya wajenge connection mpya.
“Kwenda kushot nje ni exposure, kwasababu ni kama umetoka Morogoro unafanya kollabo na msanii wa Arusha, sehemu ambayo umetoka na sehemu unayoenda ni ugenini always utaongeza kitu tu. Kwasababu kuna watu wengine wana njia nyingine za kufanya kazi na biashara. Kwahiyo muziki ni lugha ambayo popote inaeleweka, haina tabaka”, alisema Belle 9.
Pia aliongeza, “Kwahiyo ni kitu kizuri sana kolabo za nje pamoja na kufanya kazi na watu tofauti, hata kushoot video. Hapa ndani pia tuna director’s wazuri, wasanii wazuri, pia kuna wadau wazuri ambao wanaweza kuwafikisha wasanii sehemu. Tumeona wasanii wengi miaka hii ya karibuni wametusua kutokana na kujichanganya na kutojiwekea mipaka ya kufanya kazi”.
Source: Bongo 5




Leave your comment