TANZANIA: Peter Msechu adai wasanii wengi hawajui kuandika mashairi..

 

Msanii Peter Msechu baada ya kukiri kuandikiwa baadhi ya nyimbo zake, amedai wasanii wengi wa Bongo hawajui kuandika mashairi ya nyimbo zao lakini wamekuwa wakidanganya umma kwamba wanaandika wao wenyewe.

Hivi karibuni Peter alikiri kuwa wimbo wake wa ‘Nyota’ aliyoandikiwa na Amini, ni wimbo uliomletea mafanikio kuliko nyimbo zake zote.

Akizungumza katika kipindi cha Mkasi TV, Msechu alisema kuwa ufike wakati wasanii wawe huru kuweka wazi watu ambao wanafanya nao kazi.

“Wasanii wengi wa Bongo hawajui kuandika sema hawasemi wanaandikiwa, et.. hii story ya kweli imemtokea, ni uongo maana yake sio true stori”, alisema Peter Msechu.

Kwa sasa Msechu anatamba na kibao cha ‘Malava’ alichoandikiwa na msanii mwenzake Barnaba.

Leave your comment