TANZANIA: Kaa tayari kupata kolabo kati ya Alaine, Diamond na Nay Wa Mitego!

 

 

Nay Wa Mitego baada ya kuachia wimbo wa ‘Shika Adabu Yako’ na kufungiwa na Baraza la Sanaa Taifa(BASATA) ameshare picha kwenye ukurasa wake wa Instagram akiwa na Alaine wa Jamaica, Diamond Platnumz, Tudy Thomas, meneja wa Diamond Sallam na wengine wakiwa Studio. Picha hiyo ikionyesha ishara ya kurekodi kibao kipya na mrembo huyo wa Jamaica.

Mrembo Alaine amekuja Afrika Mashariki wiki iliyopita na anatarajia kuzindua albamu yake mpya iitwayo ‘Ten of Hearts’ huko jijini Nairobi, Kenya.

Pia hii ni mara yake ya pili kuja nchini, mara yake ya kwanza ilikuwa mwaka 2013 kwenye Fiesta ya Dar es Salaam.

 

Leave your comment