TANZANIA: Ray C alalamikia magazeti ya udaku jinsi yanavyomuumiza mama yake!
22 February 2016

Mwanamuziki Rehema Chalamila maarufu kama Ray C amesema mama yake amekuwa akipatwa na presha mara kwa mara kutokana na habari anazoziona kwenye magazeti ya udaku kwamba mwanaye amerudia matumizi ya dawa za kulevya.
Akizungumza katika kipindi cha Planet Bongo cha East Africa Television, Ray C amesema mama yake hana amani kutokana na mambo yanayoandikwa na magazeti ya udaku.
“Mimi naweza nikasema nakushtaki, wewe una hela zaidi na unaweza ukanishinda, your powerful get a gun watu wanifyatue na wampige na mama yangu, maana mama yangu yupo hospitali na ana presha kwasababu ya gazeti lake”, alisema Ray C.
Wiki kadhaa zilizopita gazeti la Ijumaa liliandika habari kuwa mwanadada huyo alionekana mazingira fulani ambayo yanadaiwa kupatikana madawa ya kulevya.





Leave your comment