TANZANIA: Nay wa Mitego kuachia video ya ‘Shika Adabu Yako’ licha ya wimbo kufungiwa!

 

Mbali na BASATA kutoa tamko la kuufungia wimbo wa “Shika Adabu Yako” wa Nay Wa Mitego, msanii huyo ametangaza kuachia video ya wimbo huo ambao amewasema watu mbalimbali.

Nay amesema video hiyo itatoka rasmi Ijumaa ya Februari 26. Nay aliandika kwenye ukurasa wake wa Instagram kuhusu video hiyo;

“#ShikaAdabuYako 26Feb video inatoka..! Ijumaa hii.! ShikaAdabuYako”

Wiki iliyoisha BASATA ilitoa tamko rasmi ya kuufungia wimbo huo kutokana na ukiukwaji mkubwa wa maadili, kashfa, uchochezi, kudhalilisha watu na kuhatarisha amani na utengamano miongoni mwa wasanii na jamii kwa ujumla.

Leave your comment