TANZANIA: Mwana FA hufanya boxing kwa kujifurahisha!

 

Msanii wa muziki wa Hip hop, Mwana FA ameeleza kuwa hana nia tena ya kuendelea kucheza boxing kwasababu kufanya hivyo kunaweza kumdhuru.

Msanii huyo ameweka wazi kuwa ni mizuka tu kutoka na kuzungukwa na mchezo huo ukizingatia mtaani kwao huko Tanga walikuwa wakicheza mchezo huo.

“Nilitaka kupanda ulingoni kabisa lakini nikafikiria nikaona dah, unaweza ukakalishwa, ukawa unauza magazeti mwaka mzima ..sina sababu ya kufanya boxing kama proffesion… kila mtu mtaani kwetu anapigana ngumi kwaiyo ilikuwa ni mchezo ya utakutana nao tu ukikua”, alisema Mwana Fa na kuongeza kwa sasa anafanya kwa kujifurahisha.

Source: Clouds FM

Leave your comment