TANZANIA: Rais Magufuli aagiza TRA kukamata kazi feki za Wasanii!

 

Raisi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli Alhamisi hii alikutana na makundi mbalimbali yaliyoshiriki kwenye kampeni za uchaguzi mkuu 2015 wakiwemo wasanii.

Katika hotuba yake ya makundi hayo, Magufuli ameitaka Mamlaka ya Mapato (TRA) kuhakikisha inakamata kazi feki za wasanii.

“Kama ambavyo wameweza kufanya kazi ya kushika makontena, wafanye na huku kwa operesheni maalumu kwa kazi za wasanii ambazo hazina stika na washughulikiwe ili serikali ipate mapato yake lakini na wasanii wapate haki yao. Nataka niwahakikishie ndugu zangu waandishi, wasanii na wanamichezo kwa ujumla tulianza wote wakati wa kampeni na ni lazima tumalize wote”, alisema Mh. Rais Magufuli.

Ni muda mrefu wasanii wamekuwa wakilalamika kuhusu kuibiwa kazi zao huku wakihimiza serikali kuandaa sheria kali ambazo zitalinda kazi za wasanii.

Leave your comment