TANZANIA: Lady Jay Dee hatimaye apata talaka yake baada ya miaka 9 ya ndoa!

 

Hatimaye Lady Jay Dee apata talaka yeke baada ya mvutano wa muda mrefu na mume wake Gadner Habash.

Mwanamuziki huyo Judith Wambura Mbibo maarufu kama Jay Dee, amepata talaka hiyo katika mahakama ya Manzese huko Sinza jijini Dar es salaam. Wanandoa hao wamepata talaka yao mwishoni mwa wiki iliyopita na kuwa huru kila mmoja na maisha yake.

Wanandoa hao walitengana miaka miwili iliyopita, ni baada ya miaka zaidi ya 9 kwenye ndoa. Jay Dee aliyeimba vibao mbalimbali kama Yahaya na Distance amedai mume wake ni msaliti.

Katika mahojiano yake yaliyopita na Word alisema, “Sikuweza kuendelea na ndoa yangu, sikuwa na furaha muda wote na ndio maana nikaamua kuimaliza, Mume wangu alikuwa akinisaliti na kunywa pombe kupita kiasi, wakati nilikuwa nikifanya kazi kwa bidii na kuupa uhusiano wetu nafasi kwa ninavyoweza. Ninashukuru na furaha kwa kuwa hatuna watoto pamoja”.

Gadner ambaye ni mtangazaji wa kituo cha redio cha E Fm, amekuwa kimya kwa tuhuma zote hizo bila kusema kitu chochote.

Lady Jay Dee siku ya harusi yake na Gadner Habbash wakiwa ndugu na marafiki wa karibu.

Source: The Star

Leave your comment