TANZANIA: Kampuni ya Unity Entertainment haisimamii wasanii – AY
17 February 2016

Msanii wa Hiphop nchini, Ambwene Yesaya ambaye ni CEO wa kampuni ya Unity Entertainment amesema kampuni yake haisimamii wasanii kama wengi wanavyodhani.
AY ameyasema hayo kwenye 255 ya XXL ya Clouds FM Jumanne hii, alisema Unity ni kampuni ya uwakala.
“Unity haisimamii wasanii”, alisema AY.
“Tuna focus kwenye kona nyingine zaidi, kutengeneza matangazo na kuwa wakala wa kazi zingine za muziki, kuconnect wasanii, kuleta waanii kutoka nje, kuconnect na directors wanaoweza kufanya matangazo ya TV”, aliongeza AY.
AY alisema pia kuwa kuna kampuni mpya anaanzisha ambayo itakuwa inasimamia wasanii.
“Kuna kampuni nyingine inakuja na itasimamia wasanii, unajua unapoamua kumsimamia msanii unatakiwa uhakikishe anasonga mbele”,alisema AY.




Leave your comment