TANZANIA: Vanessa Mdee atangaza nafasi ya kazi “Msaidizi wake”
17 February 2016

Muziki ni ajira, na pale ambapo wasanii hufanikiwa kutokana na shughuli zao za Sanaa, kupitia wao wana nafasi ya kusaidia vijana wenzao kwa kuwapa ajira kutokana na Sanaa yao.
Vanessa Mdee ni brand inayoendelea kukua ndani na nje ya Tanzania, kwasababu hiyo msanii huyo wa “Never Ever” ameamua kutoa nafasi ya kazi (ajira) ya Msaidizi Mkuu (PA- Personal Assistant).
Kupitia ukurasa wake wa Instagram Vanessa ameshare na mashabiki tangazo hilo la ajira;

Hii ni hatua na jambo zuri kwa msanii, kwasababu kwa kupitia mafanikio ya wasanii ni vijana wengi wataweza pia kujipatia kipato na kuweza kuendeleza ujuzi wao kupitia Sanaa. Hongera kwa Vanessa Mdee, vijana hii ni nafasi yenu kuweza kufanya kazi na msanii huyu.
Kwa taarifa zaidi tembelea tovuti yake www.vanessamdee.com .




Leave your comment