TANZANIA: Gosby atoa sababu za Hiphop ya Tanzania kutofanya vizuri Afrika!

Rapper Gosby ameelezea sababu anazohisi zinapelekea hip hop ya Bongo kushindwa kufanya vizuri Afrika.

Akihojiwa na tovuti ya Bongo 5, Gosby amesema muziki wao unafanya vizuri kwakuwa wengi wamesoma na kuna wanigeria zaidi ya milioni 50 walio nje ya nchi ambao hurudi na kuwekeza kwenye muziki.

Amesema wao waliamua kuwatengeneza wasanii wao wa hip hop kuwa wakubwa na kuwapa nguvu na heshima. Na kuongeza kuwa kwa Tanzania hiphop bado haijapewa baraka za kutosha na inaendelea kuchukuliwa kama ni uhuni.

“Hata ukiangalia kwenye corporate events, ni wasanii wachache sana wa hip hop wanaitwa, wengi wanaitwa wa kuimba”, amesema Gosby.

Pia amesema kuwa wasanii wengi wanaopewa ubalozi ni wale wanaoimba ukilinganisha na wasanii wa hiphop.

Source: Bongo 5

Leave your comment