TANZANIA: AY awataka wasanii wakongwe kwenda na wakati ili kufanikiwa!

 

Msanii mkongwe wa muziki wa Hip Hop nchini, Ambwene Yesaya maarufu kama AY amesema wasanii wegi wakongwe wameshindwa kufanya vizuri kwenye muziki wa sasa kutokana na kushindwa kubadilika na kwenda kisasa.

Akizungumza kwenye kipindi cha Mkasi TV Jumatatu hii, AY alisema mabadiliko ni muhimu kwa kila msanii anayehitaji kwenda mbali zaidi.

“Kuna aina mbili ya kupokea maoni kutoka kwa mashabiki, mtu anaweza akakwambia oya AY ulivyochana kwenye Raha Tu baki pale pale, sasa kuna wasanii wengine wanachukua vilevile bila kujua muziki unabadilika kutokana na wakati”, alisema AY.

“Maisha ya binadamu sio kwenye muziki tu, hayawezi kwenda bila kubadilika. Kwahiyo wasanii hawapendi kubadilika, akishachukua maoni anayashikilia hayo hayo basi na yeye anabaki hapo hapo. Alianza kuimba nyimbo ya aina fulani basi atashikilia hapo hapo, hicho ndicho kinachowacost, kwahiyo unamkuta mtu anaanza kulaumu media bila kujua hata media zinaenda na mabadiliko”, aliongeza AY.

Msanii huyo kwa sasa anafanya vizuri na Remix ya wimbo wake wa Zigo aliomshirikisha Diamond Platnumz.

Leave your comment