TANZANIA: Msanii John Woka afariki dunia.

 

Msanii wa muziki aina ya rap kwa design ya kama mlevi, Michael Dennis Mhina maarufu kama John Woka amefariki dunia alfajiri ya Jumanne ya leo.

John Woka amefariki baada ya kulipukiwa na mtungi wa gesi juzi, alikuwa amelazwa kwenye hospitali ya taifa ya Muhimbili jijini Dar es salaam.

Hii ni taarifa fupi iiyotolewa na mtu wa karibu wa kuelezea ajali hiyo;

Walikuwa wanahangaikia kurekebisha usafiri kwenye garage hapo Sinza, sasa katika kuhangaika upande wa AC mtungi wa gesi ukalipuka, moja ya vipande vya chuma vyenye ncha kali kikamchoma kichwani.

Kwa yeyote aliyeguswa na angependa kutoa rambirambi anaweza kuwasiliana na Omary ambaye ni kaka yake kwa nambari hizi +255767007005.

Mungu ailaze roho ya marehemu peponi.. Amin.

Leave your comment