TANZANIA- Dogo Janja adai Tip Top imepanga kumfelisha!
16 February 2016

Msanii wa HipHop, Dogo Janja huwenda akawa hawaelewani na uongozi wake wa Tip Top connection baada ya kuzagaa kwa audio katika mitandao ya kijamii ambayo ndani yake anaeleza sababu ya kutosikika.
Kwenye audio hiyo ambayo imesambaa katika mitandao mbalimbali, inasikika sauti ya Dogo Janja wakati akimtongoza mwanamke huku akimweleza sababu ya kwanini hatoi nyimbo.
“Sometimes nahisi kama vile wakina Tale, Madee,k kina Tunda wananibania fulani, nahisi wamenirudisha kundini ili wanipoteze. Kwasababu toka nimerudi Tip Top nina mwaka na nusu, nimefanya nao show nyingi ila ndio hivyo wanabana, huoni hadi Ray kaikimbia yuko zake WCB uko”, alisema Dogo.
Dogo Janja aliongeza na kusema hapati msaada wowote kutoka Tip Top Connection na kudai bora wangemwacha peke yake ajue moja kuliko kukaa na adui anakuchekea.




Leave your comment