TANZANIA: Tutetee maslahi ya jamii kupitia muziki wetu – Mwana FA

Mwanamuziki wa Hip Hop, Mwana FA amesema hawezi kuwaunga mkono wasanii wanaopoteza misingi ya muziki huo kwa madai ya kuweka mbele maslahi na kuacha changamoto zinazoikabili jamii.

Akizungumza katika kipindi cha Planet Bongo cha East Africa Radio, Mwana FA alisema kuwa wasanii wanataka kufanya vitu ambavyo hawana uhakika navyo kama vinaingiza fedha nyingi.

“Muziki umebadilika sana, umetoka katika ile misingi iliyowekwa sababu zake kuwapo, umekuwa starehe na hela peke ake”, alisema FA.

“Yaani ile misingi imebadilika sana, na vitu vingi ambavyo vilikuwa vinapingwa vilionekana vya kipumbavu mwanzoni huko, sasa hivi ndio kama mtindo, watu wanafanya watakavyo kwasababu wanataka kutengeneza pesa tu..”, aliongeza.

Pamoja na hayo, Mwana FA amesema anajua muziki umekuwa biashara lakini ni lazima misingi izingatiwe.

“Muziki umekuwa biashara kiukweli, kama unaleta hela kwanini watu wachukie hela zao lakini ninachopinga ni kuipoteza kabisa misingi ya Hip Hop kwasababu ye hela”.

Leave your comment