TANZANIA: John Woka apata ajali mbaya ya kulipukiwa na gesi, Yupo ICU Muhimbili!

 

Rapa maarufu ajulikanaye kwa style ya kurap kama amelewa, John Woka, amepata ajali ya kulipukiwa na mtungi wa gesi. Kwa sasa amelazwa kwenye hospitali ya taifa Muhimbili jijini Dar es salaam.

Hii ni taarifa iliyotolewa na mtu wa karibu wa msanii huyo;

Walikuwa wanahaingaika kurekebisha usafiri kwenye garage hapo Sinza, sasa katika kuhangaika upande wa AC mtungi wa gesi ukalipuka, moja ya vipande vya chuma chenye ncha kali kikamchoma kichwani. Madaktari wanahofia imefika mbali kiasi kwamba damu inamwagikia kwenye ubongo.

Mpaka hapa bado hajapata fahamu, mipango ya matibabu bado inaendelea. Tunasubiri kuambiwa kinachotakiwa kufanyika na mahitaji. Hospitali pale yupo kaka yake ambaye anapatikana kwa number ya Woka +255767 007005 na mzee wake, kwa yeyote ambaye angependa kufika, kujua kinachoendelea au kuchangia chochote anaweza kumpigia tu moja kwa moja

Source: Bongo 5

Leave your comment