TANZANIA: Nay wa Mitego aonywa na ex wake baada ya kumuweka kama Valentine wake!

Katika siku ya Valentine kila mtu huchagua yule amtakaye kuwa valentine wake, basi msanii Nay wa Mitego aliamua kumchagua aliyekuwa ex wake, suala ambalo ex wake huyo Shamsa hakufurahishwa nalo kabisa.

Mrembo huyo hakufurahishwa na kitendo cha Nay kumpost katika ukurasa wake wa Instagram kutokana na kwamba yeye kwa sasa yupo mikononi mwa mwanaume mwingine, hivyo Shamsa aliamua kuandika hivi;

“Naona mambo yanaendelea kuvumishwa kwamba nimerudiana na Nay. Pls pls nina maisha yangu na mwanaume ambaye nampenda na kumuheshimu …sijarudiana na Nay na haiwezi kutokea kabisaaa”, aliandika Shamsa.

“Nay una ndugu na marafiki wengi wakuwapost siku ya leo, haikuwa muhimu unipost mimi. Nilishukuru Mungu watu walishasahau kuhusu mimi na ww but naona umeyataka kuyafufua. Sipendi scandal na si maisha yangu kutafuta kiki za kijinga. KAZI YANGU NDO INAYONITAMBULISHA..PLS TUHESHIMIANE”, aliongeza Shamsa.

Shamsa Ford na rapa Naya Wa Mitego waliwahi kuwa na mahusiano yaliyodumu kwa muda mfupi tu.

Leave your comment