TANZANIA: BASATA yaifungia rasmi nyimbo ya Nay wa Mitego ‘Shika Adabu Yako’!

Baraza la Sanaa Tanzania latoa taarifa rasmi kuhusu kuufungia wimbo wa msanii Nay wa Mitego uitwao ‘Shika Adabu Yako’.

Kutokana na ukiukwaji mkubwa wa wa maadili, kashfa, uchochezi, kudhalilisha watu na kuhatarisha amani na utengamano miongoni mwa wasanii na jamii kwa ujumla.

Pamoja na kuufungia wimbo huo, BASATA litampa kalipio kali msanii huyo na kumwagiza kuacha mara moja kujihusisha kwa namna yeyote ya kuutangaza wimbo huo au kuusemea katika vyombo vya habari vinginevyo hatua kali zaidi na za kisheria zitachukuliwa.

Ifahamike kwamba kwa mujibu wa kifungu cha 4 (1) (j) cha sheria ya BASATA namba 23 ya mwaka 1984, Baraza limepewa mamlaka ya kuratibu na kufuatilia mienendo ya mtu yeyote anayehusika na Sanaa na kuhakikisha linalinda maadili ya kitaifa na miongoni mwa Wasanii wanapokuwa jukwaani au wanapobuni kazi yoyote ya Sanaa.

Aidha kifungu cha 4 (2) cha sheria hii kinalipa Baraza nguvu ya kisheria kufanya jambo lolote lile kuliwezesha kufanya majukumu yake kwa faida na ustawi wa taifa.

Baraza la Sanaa la Taifa limekuwa likipokea simu za maswali na malalamiko kadhaa dhidi ya tabia hii chafu kutoka kwa waandishi wa habari na wadau wa Sanaa ambao kwa njia moja ama nyingine wameguswa na kuchukizwa na kazi hiyo ambayo sit u inadhalilisha tasnia ya Sanaa bali inawafanya watu makini kuanza kuhoji hadhi ya msanii, weledi na taaluma ya Sanaa kwa ujumla.

Hii hapa taarifa kamili ya BASATA.

Leave your comment