TANZANIA: Grace Matata, Ben Pol na Patricia Hillary kutumbuiza kwenye Tamasha la Valentine Affairs!

Wasanii wa muziki, Ben Pol, Grace Matata na msanii mkongwe wa muziki wa Taarabu nchini Patricia Hillary, wanatarajia kupamba tamasha la ‘Valentine Affairs’ litakalofanyika Februari 14 (siku ya Valentine) katika ukumbi wa King Solomoni jijini Dar es salaam.

Akizungumza na waandishi wa habari Alhamisi hii katika ukumbi wa King Solomon, Mratibu wa tamasha hilo, Hellen Kazimoto alisema tamasha hilo la ‘Valentine Affairs’ litawapa nafasi wapenda burudani na wapendanao kwa ujumla kujumuika pamoja kwa ajili ya burudani na chakula chenye hadhi ya nyota tano.

“Hili onyesho litakuwa la aina yake kwasababu tutakuwa na burudani kutoka kwa Ben Pol, Grace Matata pamoja na Patricia Hillary. Pia kutakuwa na zawadi mbalimbali ambazo zitatolewa kwa wapendanao ambao watahudhuria tamasha hili”, alisema Hellen.

Hellen alisema zawadi zitakazotolewa ni pamoja na pete watakaokuwa na bahati watapata pete yenye thamani ya shilingi milioni 4 iliyotengenezwa kwa madini ya Tanzanite.

Pia alisema zawadi nyingine ni malazi ya siku mbili kwa wapendanao hotel ya Regency Park Hotel ambao pia ni wadhamini wa tamasha hilo.

Mmoja kati ya wasanii watakaotumbuiza kwenye tamasha hilo, Ben Pol amesema amejipanga vya kutosha kusherehekea pamoja na mashabiki wake.

Leave your comment