Saraha kushiriki katika mashindano makubwa ya kutangaza muziki kwa Kiswahili nchini SWEDEN!
11 February 2016

Muimbaji wa nchini Sweden, Saraha aliyewahi kuishi Tanzania kwa miaka kadhaa anatarajia kushiriki kwenye mashindano makubwa nchini kwao.
Mrembo huyo amesema kupitia mashindano hayo, atautangza muziki wa Kiswahili.
Kupitia ukurasa wake wa FaceBook Saraha ameandika, “Tarehe 20 natoa wimbo wangu mpya- Kizunguzungu! Nitaingia mashindano maarufu na makubwa ya muziki nchini Sweden! Nimepata nafasi kubwa ya kutangaza mziki wangu na mziki ya Kiswahili”.
Saraha alirudi nchini kwao Sweden baada ya kuachana na aliyekuwa mume wake, Fundi Samweli.




Leave your comment