TANZANIA: Nay wa Mitego akanusha taarifa za BASATA kuufungia ‘Shika Adabu Yako’

Rapa Nay wa Mitego amekanusha taarifa zilizoenea kuwa, Baraza la Sanaa Tanzania (BASATA) limeufungia wimbo wake aliotoka kuachia siku mbili zilizopita wa ‘Shika Adabu Yako’.

Msanii huyo ametoa ufafanuzi huo kupitia ukurasa wake wa Instagrama na kuandika haya;

Hata hivyo Februari 10 Katibu Mtendaji wa Baraza hilo amesema, Geofrey Mngereza alihojiwa na kipindi cha Planet Bongo cha East Africa Radio na kusema kuwa wimbo huo haufai.

“Ni wimbo ambao haufai na ni msanii ambaye I don’t know hata unashindwa kumpima ana akili ya namna gani, au kwanini ameamua kufanya hivyo, lakini watu kama hao kwenye jamii wapo, ni kazi ambayo haifai katika jamii kwa hiyo kwa mujibu wa sheria na kanuni zake, kitu ambacho hakifai kwenye jamii sio mpaka litolewe kwenye tamko kwamba wimbo umefungiwa, ni wimbo ambao haufai hata wanajamii wameona haufai, nadhani mtu mwenye akili timamu kiujumla anajua, najua kwenye media hauwezi kupigwa”.

“Anachokifanya afikirie yeye ni nani na ana nafasi gani kwenye jamii, kwasababu mtu anayefanya namna hii asidhani kama anamdhalilisha mtu, anajidhalilisha mwenyewe kwasababu mtu yeyote anayetoa lugha chafu, anafanya vitendo vya aibu, asidhani kama anamdhalilisha mtu, kwahiyo yeye mwenyewe ni kama hayawani tu”, aliongeza.

Katika wimbo hupo Nay amewaongelea watu wengi, akiwemo Wema Sepetu, Ommy Dimpoz, Shetta na BASATA.

 

Leave your comment