TANZANIA: Nandy ashika nafasi ya pili na kupata mil 33, pia kufanya kazi na Chocolate City kwa miezi 3!
10 February 2016

Shindano la kwanza la Karaoke barani Afrika, Tecno Own The Stage final limefanyika Jumapili ya Februari 7, huku ushindi ukiwa umeenda Nigeria kwa mrembo Shapeera.
Licha ya mshindi wa kwanza kutoka Nigeria, Tanzania nayo haikuachwa mbali na kushika nafasi ya pili kwenda kwa Nandy. Naye amejishindia $15,000 ambazo ni zaidi ya milioni 33. Pia amepata shavu la kunolewa kimuziki na label ya muziki ya Chocolate City ya nchini Nigeria. Ndani ya label hiyo pia wapo wasanii wakubwa kama Victoria Kimani, Ice Prince, M.I na wengine.

Pascla, Shapeera na Nandy
Antoneo Soul aliyekuwa mwalimu wa sauti aliwapongeza washindi hao kwa kuandika Instagaram;
“Congratulations to my mentees @mz_shapera for winning season 1 #TECNOOwnTheStage and for @nandy_babygirl for coming in second. I don’t mean to brag but damn I create superstars….And to @pascaltokodi who’s held the Kenyan flag high for coming in third and @sikindividual at fourth. I am very proud of y’all. Time to be glabal superstars now. Don’t stop fighting to reach the top. Don’t stop.”
Pia katika show hiyo Vanessa Mdee alitumbiza mbele ya watazamaji na majaji wa show hiyo, Yemi Alade, M.I na Bien.

Tazama pia baadhi ya picha katika siku hiyo ya fainali ya shindano la TecnoOwnTheStage;











Leave your comment