TANZANIA: Q Chief kufanya video Dubai na Justin Campos!

 

Msanii wa muziki ambaye yupo chini ya label QS J Mhonda, Q Chief amesema yupo kwenye maandalizi ya kusafiri kwenda kushoot video zake mbili nchini Dubai na director wa Afrika Kusini Justin Campos.

Akizungumza katika kipindi cha Planet Bongo cha East Africa Radio Jumanne hii, Q Chief amedai video hizo zinaweza kuitangaza Bend yake mpya ya ‘QJ International’ ambayo alizindua hivi karibuni.

“Mimi pamoja na uongozi wangu tunashusha video mbili, tayari tumepanga kwenda kushoot Dubai. Hizi video zitatambulisha band yangu na tutafanya na Justin Campos kwasababu ni director mkubwa barani Afrika”, alisema Q Chief.

Licha ya hayo Q Chief pia alisema kwa sasa hivi yeye pamoja na bendi yake ‘QJ Interanational’ ameweka kambi bagamaoyo ili kujinoa vizuri.

Leave your comment