TANZANIA:Baada ya kuachana, Nuh na Shilole wamekuwa maadui!

 

Mwanamuziki Nuh Mziwanda amedai kuwa kuvunjika kwa uhusiano wake na Shilole kumesababisha uadui kati yao.

Akizungumza katika kipindi cha Planet Bongo cha East Africa Radio, Jumatatu hii Nuh alidai imefikia hatua mpenzi wake huyo wa zamani Shilole amehack akaunti yake ya Instagram.

“Baada ya mapenzi kuisha mi nimekuwa adui yake, amehack akaunti yangu ya Instagram. Najaribu kuwacheki watu wa kuirudisha akaunti yangu wanashindwa kuirudisha anabana kila sehemu”, alisema Huh.

“Kuna vitu ananifanyia vidogo vidogo ambavyo vimenifanya kugundua kuwa hakuna mwanamke mzuri kwangu, alikuwa anashindwa kuonesha true color yake nimekuja kuijua baada ya kuachana naye”, aliongeza Nuh.

Pia Nuh alisema ingekuwa waliachana kwa amani na Shilole asingelazimika kuifuta tattoo ya mpenzi wake huyo, kwani niukweli usiopingika kwamba amemsaidia katika maisha yake.

“Mimi ningeiacha tattoo kama Shilole ningeachana nae poa, kila mtu na maisha yake fresh tukionana tunasalimiana hakuna noma, lakini mwenzangu kwenye interview anaongea hiki kwamba mimi sina kitu, sijui nashindwa kusurvive nakula magengeni, anaongea vitu ambavyo anajaribu kutoa fan base yangu, angekuwa mtu mzuri baada ya kuachana naye, tattoo ningeiacha kwasababu ningejua kabaki kuwa rafiki yangu na ni mtu ambaye alinisaidia”.

Nuh alimaliza kwa kusema kuwa yeye hana chuki na msanii huyo ambaye alikuwa naye kwenye mahusiano.

 

Leave your comment