TANZANIA: Watanzania tuache kubeza kazi za wasanii, soma hapa alichokiandika Director Adam Juma baada ya kuitazama Lupela!

 

 

Baada ya siku chache kutoka kwa video ya ‘Lupela’ ya msanii Ali Kiba, muongozaji mkongwe nchini Adam Juma ameyatoa yake ya moyoni baada ya kuitazama video ya wimbo huo kupitia ukurasa wake wa Instagram.

Ameamua kutoa dukuduku baada ya kuona comments za watu wengine wakiikosoa video ya ‘Lupela’.

“Lupela @officialalikiba , this is art, watanzania hatujui kuidadavua art. Hatujui thamani ya kitu, tunachukulia kiurahisi urahisi tu, kila mtu anajifanya anajua kitu ambacho sio sawa. Hii sio video tu, tulia basi angalia kwa umakini utapata ujumbe usipoelewa inawekana tatizo lipo kwenye level yako ya kuchanganua ujumbe ktk picha, btw sio fan wa alikiba ni mwana tu. Ningependa kusema video ni A one, haifanani na kitu ambacho tumezoe!!! Go kiba…...”ma – Adam Juma

Lakini baada ya post hiyo kushinda kwa siku moja tu, Muongozaji huyo wa video za muziki nchini alioga matusi ya mashabiki kwa kuisifia video ya Ali Kiba, na kuandika tena 'Jana nimeoga matusi mpaka raha aisee.... kumbe ni hivi sikujua aisee".

 

 

Leave your comment