TANZANIA: Tunda Mana kupata ubalozi wa ‘AMSHA MAMA' kupitia ‘Mama Kijacho’

 

Mwimbaji Khalid Ramadhan aka ‘Tunda Man’ kupitia wimbo wake wa ‘Mama Kijacho’ amepata dili la ubalozi wa tamasha la wanawake liitwalo ‘AMSHA MAMA2016’.

AMSHA MAMA2016, ni tamasha lililoanzishwa nchini Kenya kwa lengo la kumhamasisha mwanamke kufanya kazi kwa bidii ili kujikomboa katika mfumo dume.

Tunda Man ameiambia tovuti ya Bongo 5, jumamosi hii kuwa anamshukuru Mungu kwa kupata dili hilo.

“Hawa jamaa baada ya kuona wimbo wa ‘Mama Kijacho’ wakanitafuta, wakaniambia tumeupenda sana wimbo wako, pia tumependa uwe balozi wa tamasha la ‘AMSHA MAMA2016’

Upande wa Mkurugenzi wa tamasha hilo ambaye pia ni Mkurugenzi Mtendaji wa ‘label’ ya Candy na Candy Records ya nchini Kenya, Joe Kariuki, alisema Tunda ni msanii mzuri, hivyo wameamua kumchukua ili washirikiane nae kama balozi katika kuandaa tamasha la wanawake litakalofanyika Mwezi Machi katika Hotel ya Kifahari ya Tribe nchini Kenya.

Joe Kariuki

“Tunda ndiye balozi wetu wa tamasha kwa hapa Tanzania. Pia tutakuwa tunashirikiana nae katika matamasha mbalimbali ambayo tutayaandaa”, alisema Joe.

Leave your comment