TANZANIA: Joh Makini asema kuwa mbali na nyumbani kunafanya kufanya kazi kwa bidii zaidi, Fahamu ni kwanini ametoa kauli hiyo!

Msanii wa kundi la Weusi, Joh Makini ameeleza sababu mbalimbali zinazowafanya wasanii wanaotoka mikoani kufanya vizuri kimuziki pindi wanapofika Dar es salaam.

Rapa huyo anayehit na video ya wimbo wake wa ‘Don’t Bother’ akiwa amemshrikisha AKA wa Afrika Kusini, amekiambia kipindi cha Mkasi cha EATV kuwa wasanii wengi wa mikoani hufanikiwa kutokana na kujiona wako mbali na nyumbani.

“Unapokuwa umetoka kwenu ukaja sehemu kufanya kazi, lazima ujue hapa sio kwenu umekuja mjini. Kwahiyo lazima uhakikishe kwanza speed yako sio ya kawaida katika kazi”, alisema Joh Makini.

“Mimi wakati nimekuja Dar, nilikuwa naishi geto, na tulikuwa tunaishi kwa kubangaiza mizinga mingi na nini. Unapokuwa unaenda studio na kurudi geto unajua sio kwenu pale unaamshwa muda wowote. Huwezi fanya kazi katika speed ya kawaida kama ni mtu unayependa kazi na unajua unachokifanya. Kwahiyo mimi nafikiri labda wasanii wanaotoka mikoani wanakuja Dar es salaam wengi wanafanya vizuri kwasababu kuwa mbali na nyumbani inakusukuma kufanya kazi kwa bidii, upo hapo kwa wakati na unatakiwa kuitumia kila dakika”.

Joho Makini ambaye anatokea mkoani Arusha pamoja na wasanii wenzake wanaounda kundi la Weusi, ni miongoni mwa wasanii wa Hip Hop wenye mafanikio kwa sasa.

Leave your comment