TANZANIA: Video ya ‘Walk it Off’ ya Fid Q kuachiwa wikiend hii
5 February 2016

Fid Q akitengeneza vyema nywele zake kabla ya kushoot video hiyo mwishoni mwaka jana
Rapa Fareed Kubanda aka Fid Q anatarajia kuvunja ukimya kwa kuachia video ya wimbo wake mpya uitwao ‘Walk it Off’ aliomshirikisha Taz.
Video ya wimbo huo ilifanyika nchini Afrika Kusini mwishoni mwa mwaka jana. Imeongozwa na Nicroux wa kampuni ya Molotov Cocktail ya Afrika Kusini ambayo miongoni mwa video ilizofanya ni pamoja na Jealousy ya AKA na Rands na Nairas ya Emmy G.
Kupitia Instagram, Fid Q ameandika: #TANGAZO New visuals by Fid Q @therealfidq feat TAZ – directed by @nocroux coming your way this weekend.. stay tuned”
Video hiyo ya ‘Walk it Off’ inakuwa ni nyimbo yake ya kwanza kufanya Afrika Kusini.




Leave your comment