TANZANIA: Kajala asema Bongo Movie wana uwezo wa kumshitaki Nay Wa Mitego!
4 February 2016

Rapa Nay Wa Mitego baada ya kupost katika mitandao ya kijamii mashairi ya wimbo wake mpya yenye ‘utata’ hivi karibuni, mmoja kati ya wasanii wa Bongo Movie Kajala Masanja ametishia kumshitaki mahakamani.
Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Ney Wa Mitego aliandika;

Baada ya kauli hiyo, Kajala aliiambia Clouds FM kuwa hawajafurahishwa na kauli ya Nay.
“Nyie mnacheka mnaona sifa huyo anatukana. Wakati sisi Bongo Movie wote tunao uwezo wa kumshtaki, hawezi kututukana hivyo yeye ni nani? Mnakaa mnadhalilishwa mnafurahi? Alisema Kajala.
Hata hivyo msanii Nay alijibu kauli kwa kusema,
“Nimesikia kuwa Bongo Movie wana mpango wa kunipeleka mahakamani, nimeongea na wakili wangu kaniambia tutshinda kesi. Halafu Kajala namuheshimu kama mama yangu, nimesikia alichosema nasubiria wanipeleke mahakamani” alisema Nay.




Leave your comment