TANZANIA: Kolabo Yetu na Diamond ni hatari sana – Mafikizolo

Kundi la muziki la Afrika Kusini, Mafikizolo limedai kuwa kolabo yao na Diamond Platnumz (Tanzania) iitwayo ‘Colours of Africa’ ni moto wa kuotea mbali (hatari sana).

Mmoja wa kundi hilo, Theo amedai hadi sasa video yake hadi sasa haijatoka kwakuwa wamepanga kitu kikubwa zaidi kwaajili ya kuifanyia promotion.

Theo alikuwa akimjibu shabiki aitwaye Frankestain Pastory, aliyemuuliza Instagram sababu za kuchelewa kwa video hiyo.

 

“Tunafahamu kuwa mashabiki wetu wanasubiri lakini tuna mpango mkubwa wa kimasoko kwaajili ya uzinduzi wa video”, aliandika Theo.

“Mafikizolo na Diamond ni wanamuziki wakubwa sana Afrika hivyo uzinduzi wa wimbo na video yake unatakiwa kupangwa vyema. Ninachoweza kukuahidi ni kuwa video na wimbo vimesimama. Hatutowasubirisha kwa muda mrefu sana. Tafadhali kaka yangu kuwa mvumilivu, subira yako haitapotea bure”.

 

Leave your comment