TANZANIA: Diamond asaini dili nono na Vodacom na kusindikizwa na Baby Mama wake, Zari!
4 February 2016

Msanii mkubwa wa muziki nchini, Diamond Platnumz amesainhi dili nono na kampuni ya Vodacom.
Msanii huyo alisindikizwa na mzazi mwenzie Zari kwenye tukio hilo lililofanyika leo jijini Dar es salaam. Msanii huyo ambaye ni balozi wa Vodacom Tanzania hadi sasa haijajulikana mkataba wa aina gani na atalipwa shilingi ngapi lakini vyanzo vimesema Diamond amevuta pesa ndefu.
“Closed the Deal with Vodacom …watch this space! @ianferrao”, aliandika meneja wake, Babu Tale.
Kwa kuanza Diamond atahusika kwenye promotion mpya ya kampuni hiyo iitwayo Ongea Deilee, kampeni itakayowapa wateja saa 1 la kuongea bure kabisa
.
Mkurugenzi Mtendaji wa Vodacom, Ian Ferrao(wapili kushoto), Balozi wa Vodacom Tanzania, Nassib Abdul(Diamond), Kaimu Mkurugenzi wa Uhusiano na Mawasiliano wa Vodacom, Rosalynn (Kulia) na Zarina Hassan (wakwanza kushoto).




Leave your comment