TANZANIA: Sugu amtaka Rais Magufuli asafiri nje ya nchi kuona dunia inavyoenda!

Mbunge wa Mbeya mjini na mwanamuziki mstaafu, Sugu anahisi  sasa ni muda muafaka wa Rais Magufuli akapanda ndege na kwenda nchi za nje kuona namna ambavyo nchi zingine zinaendesha uchumi wake na mambo mengine.

Bwana Joseph Mbilinyi amesema safari za nje sio tatizo na kwamba baadhi ya gharama haziepukiki.

“Ili twende sambamba na dunia, sisi sio kisiwa, ni lazima Rais Magufuli aende UN, lazima aende AU kwenye vikao vya kimataifa. Sasa hivi kuna mkutano Davos wa kimataifa, dunia yote ipo kule inazungumzia uchumi yeye amekaa huku”, alisema Sugu Bungeni wiki hii.

“So President Magufuli has to go abroad, akajifunze, take a jet brother, he has to take a jet akajifunze dunia inafanya vipi, marais wengine wanafanya vipi”, aliongeza Sugu.

Sugu alidai kuwa safari za nje kwa Rais ni muhimu ila anachotakiwa ni kupunguza tu watu watakaoongozana naye.

Tangu aingie madarakani, Rais Magufuli hajawahi kusafiri nje ya nchi.

Leave your comment