TANZANIA: Usipitwe na hii hapa 'ushauri wa Shilole kwa wasanii wakike wanaotaka mafanikio'

Msanii wa muziki, Shilole ametoa ushauri kwa wasanii wakike wanaotaka pamoja na mbinu mbalimbali ambazo zitawafanya kuwa wasanii wakubwa wamuziki.

Mwanadada huyo akiwa kati ya wasanii wakike wenye mafanikio kimuziki, amekiambia kipindi cha Planet Bongo cha East Afrika Radio kuwa ili msanii afanikiwe anatakiwa kujituma zaidi.

“Wasanii wengi wakike wanashindwa kufika pale wanapotaka kwasababu hawako serious” alisema.

“Mimi kazi yangu naifanya ndio kila kitu, bila kuimba vizuri, bila kudance vizuri, bila kufanya video kali, watoto wangu watakufa njaa. Unajua sometime wasanii wakike tunajibweteka tukishatoa ngoma moja tunaona hii ndio itanivusha 2016, hapana unatakiwa uendelee kukomaa yaani kila siku wewe uwe ni mtu wa kuhangaika kurecord kazi mpya, kwa sababu lazima uwe na ngoma nyingi kwenye library ili ukitaka kutoa ngoma unachagua ngoma moja kali”.

Pia mrembo huyo aliongeza, “Kitu kingine tusibweteke na umaarufu tunaopata, tufanye kazi vilevile tuwe tunatunza pesa ambazo tunapata. Pia tusitegemee wanaume, kwasababu ukishakuwa maarufu wanaume wengi watakufuata, sasa unatakiwa ujitambue wewe ni nani”.

Leave your comment