TANZANIA: Mpoto asema akipewa nafasi ya kushika wizara ya utamaduni angehakikisha ulimwengu ungejua utamaduni wa Tanzania

Msanii wa muziki wa asili, Mrisho Mpoto amesema kama angepata nafasi ya kuteuliwa na kuwa katika Wizara ya Habari, Tamaduni na Michezo basi angehakikisha ulimwengu unaujua utamaduni wa Tanzania.

Akizungumza katika kipindi cha Papaso cha TBC FM, Mpoto alidai Tanzania bado haijanufaika vizuri na utamaduni wake.

“Mimi ningependa Wizara ya Habari, Tamaduni na Michezo kwasababu nataka kuuambia ulimwengu tuna makabila 120, tuna lugha 132, tuna vyakula, tuna mavazi, tuna kila kitu, huu wote ni mtaji tosha lakini havijulikani katika nyanja za kimataifa, tumevikalia sisi wenyewe”, alisema Mpoto.

“Kwahiyo mimi ningelichukulia swala zima la utamaduni kwasababu Tanzania tuna vitu vingi sana lakini vinapotea”, aliongeza Mpoto.

Leave your comment