TANZANIA: Ben Pol adai kabla ya mwezi mei kupita ataachia albam mpya na video za kimataifa!
3 February 2016

Msanii wa muziki wa R&B, Ben Pol amejipanga kuachia albam mpya pamoja na video mbili za kimataifa kabla ya mwezi Mei mwaka huu.
Akizungumza katika mahojiano na tovuti ya Bongo 5, Ben Pol alisema albam hiyo itakuwa na nyimbo kumi na mbili (12).
“Mwaka huu kusema kweli kuna mipango mikubwa kidogo ukilinganisha na mwaka jana na miaka iliyopita” alisema Ben.
“Watu wategemee video mbili nzuri kwenye miezi sita hii ya kwanza ambazo zinaweza kuchezwa popote duniani. Pia watu wategemee album yangu mpya, itakuwa na nyimbo 12, hiyo ni rasmi kabisa naisema. Bado sijaipa jina lakini kuna majina ambayo bado nayafikiria lakini watu wajue itatokea tena katika nusu hii ya kwanza ya mwaka”.
Pia Ben Pol amewataka mashabiki wa muziki wake kuisubiria albam yake hiyo kwani ndani yake kutakuwa na zile kolabo ambazo amekuwa akizizungumzia mara kwa mara.




Leave your comment