TANZANIA:Msechu na Ben Pol watoa zawadi ya Valentine kwa mashabiki wao

Waimbaji mahiri wa muziki Tanzania, Ben Pol na Peter Msechu wameachia ‘Mash-up collaboration’ ya nguvu iitwayo ‘Nyota ya Samboira’ kama zawadi ya msimu huu wa Valentine kwa mashabiki wao wa dhati.

“Nyota ya Samboira ni muunganiko wa nyimbo mbili, ‘NYOTA’ ya Peter Msechu na ‘SAMBOIRA’  ya Ben Pol zilizoweka historia kila moja kwa kufanya vizuri zilipotoka.

Kuhusu Mash-up hii Ben Pol amesema, “Katika msimu huu wa Valentines, mimi na Msechu tumeona tuwaunganishe mashabiki wetu wawe kitu kimoja kama ishara ya upendo, kwa kuwaletea ‘nyota ya samboira’ ambayo ni muunganiko wa kazi zetu mbili zilizofanya vizuri. Hivyo ni matumaini yetu kwamba wataendelea kusambaza upendo kwa wawapendao kupitia zawadi hii”.

Samboira ni moja ya hits za Ben Pol iliyotoka mwaka 2011 na inayopatikana kwenye album yake ya kwanza ‘MABOMA’. Nyota ni wimbo wa Peter Msechu uliofanya vizuri sana mwaka jana 2015 ambao uliachiwa mwaka 2014 mwishoni. Pia Samboira ni jina la msichana aliyeimbwa kwenye wimbo wa Ben Pol, na Nyota ikiwa na maana kama ilivyo nyota ing’aayo angani.

Sikiliza zawadi hiyo ya Valentine hapa chini;

Leave your comment