TANZANIA: Wasanii wa kike tuwe makini na wanaume wachwarwa – Mwasiti

 

Msanii wa muziki, Mwasiti amewataka wasanii wa kike wanaoingia kwenye muziki kuwa makini na wanaume wachwara ambao wanadai wanataka kuwasaidia kimuziki kumbe wanataka kuwatumia kimapenzi.

Akizungumza katika kipindi cha Bongo Beatz cha Star TV jumanne hii, Mwasiti alisema wasanii wakike wanatakiwa kujua wamefata nini kwenye muziki na kuacha kupapatikia mambo makubwa.

“Mimi nafikiri kwanza watoto wakike wajue wamefata nini kwenye muziki. Hii Sanaa ni pana sana na ina watu tofauti tofauti sio unavyowaona wasanii wankuwa wakubwa ukadhani ni kitu rahisi” alisema Mwasiti.

“Kwahiyo mabinti wanavyoingia huku sio sehemu nyepesi kama wanavyofikiria kwamba ukiingia huku utapata watu wenye pesa na mabuzi wakukusaidia, watakutumia alafu watakuacha. Kwahiyo mnavyoingia huku mjue nini kimewaleta, vinginevyo wataondoka hata walivyovijia wasivipate”, aliongeza.

Leave your comment