TANZANIA: Afande Sele aacha wosia akifa achomwe moto!
2 February 2016

Msanii mkongwe nchini Afande sele amesema kuwa ameacha wosia kwa ndugu zake akifa asizikwe bali achomwe moto.
Akizungumza katika kipindi cha Planet Bongo cha East Africa Radio, Afande Sele alisema ana imani kuwa akichomwa moto atakuwa malaika na sio kuwa binadamu tena.
Pia Afande alidai amechoka kuwa binadamu anataka kuwa Malaika ndio maana anahitaji kuchomwa moto ili siku ya ufufuo arudi kama Malaika na si Binadamu, imani yake inamtuma kuwa akizikwa kwenye udongo siku ya ufufuo atarudi kuwa binadamu tena jambo ambalo yeye hataki kulisikia tena.




Leave your comment