TANZANIA: Mwasiti kujaribu kufanya Hip Hop!

Msanii wa muziki nchini, Mwasiti Almasi amesema Fid Q, Mwana FA pamoja na Godzilla wamemwambia wapo tayari kumwandikia wimbo wa Hip Hop ili na yeye aonyeshe uwezo wake katika muziki huo.

Muimbaji huyo alikiambia kipindi cha Siz Kitaa cha Clouds TV ana nia ya kubadili muziki wake kidogo ili kupata ladha nyingine.

“Mimi napenda Hip Hop sana sema sijawahi kujaribu” alisema Mwasiti.

“Nitajaribu kuachia wimbo kwasababu nimepata bahati Mwana FA kasema ataniandikia, Fid Q amesema ataniandikia, Nikki wa Pili pamoja na Godzilla wapo tayari kuniandikia. Sasa ni mimi tu nikamilishe halafu niseme lini itatoka”, aliongeza Mwasiti

Leave your comment